FURSA Za Ufadhili Wa Masomo Nchini Indonesia Kwa Watumishi Wa Serikali 2025/2026



FURSA Za Ufadhili Wa Masomo Nchini Indonesia Kwa Watumishi Wa Serikali 2025/2026

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

FURSA ZA UFADHILI WA MASOMO (SCHOLARSHIP) NCHINI INDONESIA KWA WATUMISHI WA SERIKALI KATIKA NGAZI ZA DIPLOMA, SHAHADA NA SHAHADA YA UZAMILI KWA MWAKA WA MASOMO 2025/2026

Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Indonesia unapenda kuwajulisha kuhusu kuwepo kwa fursa za ufadhili wa masomo (scholarship) nchini Indonesia kwa Watumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika ngazi za Diploma, Shahada (Bachelor) na Shahada ya Uzamili (Masters) chini ya ufadhili wa Serikali ya Indonesia kupitia mpango wake wa Ufadhili wa Masomo wa The Indonesian AID Scholarship (TIAS) kwa mwaka wa masomo 2025/2026 katika fani mbalimbali.

Aidha, Serikali ya Indonesia itagharamia ada, posho ya kila mwezi, bima ya afya, nauli ya ndege Tanzania-Indonesia-Tanzania, mafunzo ya lugha na utafiti (Research) kwa watumishi wa Serikali kutoka Tanzania Bara na Zanzibar watakaochaguliwa kushiriki katika mafunzo hayo.

Taarifa zaidi kuhusu uchaguzi wa fani (courses) pamoja na vyuo zinapatikana kupitia tovuti ya https://tias.kemenkeu.go.id/landing/.

Aidha, waombaji watatakiwa kuwasilisha maombi yao Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwaajili ya nomination kabla au ifikapo tarehe 04 Mei, 2025.

Upatikanaji wa fursa hii adhimu kwa Tanzania ni sehemu ya mafanikio ya Ziara ya Kitaifa ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliyofanyika nchini Indonesia mwezi Januari, 2024 pamoja na mazungumzo kati ya Mheshimiwa Dkt. Hussein A. Mwinyi, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na Bw. Tormarbulang L. Tobing, Afisa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Indonesian Aid yaliyofanyika pembezoni mwa Mkutano wa Pili wa Jukwaa la Indonesia na Afrika mwezi September, 2024 Bali, Indonesia.


Sultan Uwezo

In our hands you will find out Songs and Videos of Various Artists without forgetting News from Newspapers. Here you will also find Employment's Information from the Government and the Private Sectors.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Contact Form