VITUO VYA USAILI AJIRA ZA POLISI APRIL 2025
Jeshi la Polisi Tanzania Lina waalika wasailiwa wote waliochaguliwa kufanya usaili baada ya kupita kwenye maombi ya Ajira za Polisi mwaka 2025
Hivi hapa vituo vya Usaili kwenye ajira hizo
TARATIBU ZA USAILI KWA KATEGORIA MBALIMBALI ZA ELIMU
1. Waombaji Walio na Shahada, Stashahada na Astashahada (Diploma na Cheti):
Kwa vijana waliohitimu katika ngazi ya elimu ya juu, yaani Shahada, Stashahada na Astashahada, wanatakiwa kuhudhuria usaili jijini Dar es Salaam.
Usaili huu utafanyika katika eneo la uwanja wa gwaride uliopo Kambi ya Polisi (Police Barracks), barabara ya Kilwa, nyuma ya kituo cha Polisi cha Kilwa Road.
2. Waombaji Waliohitimu Kidato cha Nne na Kidato cha Sita:
Kwa wale waliohitimu sekondari (yaani kidato cha 4 na 6), usaili wao utafanyika katika mikoa waliyowasilisha kama chaguo la eneo la usaili walipokuwa wanajaza fomu ya maombi mtandaoni. Hii inamaanisha kuwa kila msailiwa atafanyiwa usaili katika Mkoa wa Kamanda wa Polisi waliouchagua awali.
3. Waombaji Kutoka Zanzibar:
Kwa vijana wanaotoka visiwani Zanzibar, ratiba ya usaili imepangwa kama ifuatavyo:
- Kwa walioko Unguja: Usaili utafanyika katika Makao Makuu ya Polisi Zanzibar (eneo la Ziwani).
- Kwa walioko Pemba: Watatakiwa kufika katika Ofisi ya Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kusini Pemba (eneo la Chakechake).
VITU VYA KUWASILISHA WAKATI WA USAILI
Kila msailiwa lazima afike na nyaraka zifuatazo siku ya usaili:
- Vyeti halisi vya elimu (Academic Certificates)
- Cheti cha kuzaliwa
- Kitambulisho cha Taifa cha NIDA au namba ya NIDA
- Nguo na viatu vya michezo (kwa ajili ya mazoezi ya vitendo)
Kumbuka: Msailiwa yoyote atakayewasili baada ya tarehe 28 Aprili 2025 hataruhusiwa kushiriki katika usaili. Hivyo, ni muhimu kufika mapema kwa mujibu wa ratiba husika.